Have a question not answered here? Please email relief@immigrantreliefwa.org
To apply for the relief fund, you must:
Maombi yatakubaliwa kwa msingi wa atakayetuma maombi wa kwanza ndiye atakayehudumiwa wa kwanza kwa sababu jumla ya hazina ya msaada ni mdogo. Tutawapa kipaumbele wale wanaohitaji msaada zaidi.
Ndio, kila mtu anayetoka kwa nyumba yako na ana miaka kumi na nane au zaidi anastahiki kupata msaada wa hazina na anaweza tuma maombi. Kila mtu ni lazima ajaze fomu yake binafsi ya kutuma maombi. Ufadhili hautatolewa kwa zaidi ya watu watatu katika kila nyumba (malipo ya juu zaidi ni dola elfu tatu kwa kila nyumba)
Ndio. Mfuko wa Usaidizi wa Maafa wa Seattle wa Wahamiaji ni kwa watu wanaoishi Seattle.Washington RVR-19 Mfuko wa Usaidizi ni kwa mtu yeyote huko Washington.Ukiishi Seattle, unaweza kuomba pesa zote mbili.
Unaweza tuma maombi kwa kutumia mtandao, kupitia simu, au kwa kutuma barua. Njia zote tatu zinapatikana kwa Kiswahili. Siku ya mwisho ya kutuma maombi ni Disemba tarehe 6.
Kabla ya kuomba, unapaswa:
Baada ya kuomba, tafadhali hakikisha uangalie kikasha chako cha barua pepe au folda ya barua pepe isiyofaa kwa uthibitisho wako. Utapata pia uthibitisho wa ujumbe wa maandishi siku utakayowasilisha maombi yako. Unaweza kuingia tena na uangalie hali ili uone ikiwa programu yako inakaguliwa na ikiwa umepewa ufadhili. Tafadhali wasilisha ombi lako mara moja tu.
Ikiwa hutaki kukamilisha kujaza maombi yako mtandaoni unaweza kuchapisha fomu yako ya maombi hapa na kuituma kwa anwani S.L.P #84327, Seattle WA 98124
Ukikwama, piga simu kwa nambari 1-844-724-3737 (Jumatatu-Ijumaa saa tatu asubuhi-saa tatu usiku) ukihitaji msaada unapotuma maombi. Msaada unapatikana katika lugha nyingi.
Baada ya kutuma maombi, utakuwa ukipata sasisho kuhusu maombi yako kupitia barua pepe au arafa kwa simu. Utafahamishwa ikiwa maombi yako yatakubaliwa ndani ya wiki tatu baada ya kutuma maombi. Ikiwa maombi yako yatakubaliwa, utapokea malipo ndani ya wiki mbili baada ya maombi kukubaliwa.
Hazina yetu ni ndogo, kwa hivyo si kila mtu anayetuma maombi ataweza kupata msaada wakati huu.
Hizi ndizo stakabadhi unazoweza kutumia unapotuma maombi yako kudhibitisha utambulisho wako na kuwa unaishi katika jimbo la Washington.Hakikisha kuwa una nakala safi inayoonekana ya mojawapo:
Maelezo yako ya kibinafsi hayatasambazwa kwa hiari kwa serikall, ICE, watekelezaji sheria, Mpangishaji wako, mwajiri wako, au mtu yeyote. Maelezo yote yamehifadhiwa kwa njia salama Kulingana na kandarasi yetu na idara ya jamii na huduma za afya ya jimbo la Washington, Wale ambao wanauwezo wa kuona maelezo yako ya kibinafsi ni wadhamini wasaidizi,(shirika la jamii linalosimamia hazina) kituo cha Fair Work, na chama cha mikopo cha Seattle (linalosambaza pesa).Hatutasambaza habari yako kwa mtu yeyote yule. Lakini ikihitajika kisheria kuhudhuria vikao vya korti, tunaweza hitajika kisheria kupeana maelezo yako ya kibinafsi. Si rahisi hili kufanyika, lakini linawezekana.
Hazina hii inasimamiwa na mashirika ya jamii ya Washington yanayoongozwa na wahamiaji—watu wao hao ndio walioitisha kuundwa kwa hazina hii. Inaungwa mkono na kufadhiliwa na idara ya jamii na huduma za afya ya jimbo la Washington.
Hapana. Usaidizi kutoka kwa hazina hii inachukuliwa kama msaada wa wakati mmoja kwa sababu ya janga na haitazingatiwa chini ya sheria ya malipo ya umma. Kupata usaidizi kutoka kwa hazina hakutaathiri uwezo wako wa kupata kadi ya kijani.
Unaweza tuma ombi ili upate malipo ya wakati mmoja ya dola elfu moja kwa kila mtu utakayotumiwa moja kwa moja, malipo ya juu zaidi ni dola elfu tatu kwa kila nyumba. Unaweza pokea pesa hizi kama hundi au kadi ya zawad (Visa).